Guinea na Togo kucheza nje ya nchi zao kisa Ebola.
Shirikisho la Soka barani Afrika,CAF imeagiza Guinea kuandaa mechi baina yake na Togo katika taifa mbadala kufuatia mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola.Agizo hilo linamaanisha mechi baina ya timu hizo mbili zilizopangiwa kuchezwa kati ya tarehe 5-6 Septemba hazitachezwa huko .
CAF imeagiza kuwa marufuku hiyo ya mechi nchini Guinea isalie hivyo hadi baada ya mwezi Septemba.
Togo iilikuwa imeomba shirikisho la soka barani Afrika CAF kuhamisha mechi baina yake na Guinea kuenda taifa mbadala ikihofia usalama wa wachezaji wake kufuatia mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola.
Mechi hiyo iliyopangwa kuchezwa katia ya tarehe 5 na 6 Septemba ni ya kuwania kufuzu kwa dimba la mabingwa barani Afrika.
Zaidi ya watu 300 wameaga dunia kufuatia mlipuko wa homa hiyo ya Ebola nchini Guinea huku wengine zaidi ya 700 wakiaga dunia Liberia na Sierra Leone.
Shirikisho la soka nchini Togo,TFF lina uhakika kuwa serikali ya ya Togo huenda isiwaruhusu kwenda Guinea.
Mataifa mengi ya magharibi mwa afrika yamepiga marufuku mbali na kuweka mikakati ya kuzuia kuenea kwa kwa homa ya ebola ambayo kufikia sasa imewaua zaidi ya watu 1000 .
Sierra Leone inapendekeza kucheza mechi hiyo nchini Ghana.
Msemaji wa shirikisho la Ghana Ibrahim Sane ameidhibitishia meza ya michezo ya BBC kuwa wamepokea ombi kutoka Sierra Leone na kuwa wanasubiri ruhusa kutoka kwa serikali na wizara ya afya .
0 comments:
Post a Comment