Wednesday, 13 August 2014

Kijiji cha Michezo ya Olimpiki ya Vijana chazinduliwa rasmi.

Kijiji cha Michezo ya Olimpiki ya Vijana ya Nanjing kimezinduliwa rasmi jana(Agosti 12).
Mpaka jana  asubuhi, jumla ya wanamichezo 405 kutoka nchi 74, na maofisa 12 wa kamati ya Olimpiki ya kimataifa wameingia, na washiriki wengine zaidi 2300 wameingia jana.
Kijiji hicho kitahudumia wanamichezo 3,786 wakati wa michezo hiyo.
Tofauti na Michezo ya Olimpiki, michezo ya Olimpiki ya Vijana inawataka wanamichezo washiriki kwenye shughuli zote za utamaduni na elimu, na asilimia 70 ya shughuli hizo zitafanyika ndani ya kijiji hicho.

0 comments:

Post a Comment