Kieran Gibbs kukaa nje ya dimba wiki tatu.
Mchezaji wa klabu ya Arsenal anayechezea Beki upand wa kushoto Kieran Gibbs atakaa nje ya uwanja kwa wiki tatu na atakosa
mechi zote za ligi ya mabingwa dhidi ya Besiktas baada ya kuumia nyama za pajani.
Gibbs mwenye miaka 24, aliumia
wakati wa mchuano kati ya Arsenal na Crystal Palace siku
ya jumamosi.Kocha mkuu wa klabu hiyo Arsene Wenger amekiri na kuthibitisha taarifa hizo na kudai kuwa ameachwa katika kikosi kitakachocheza UEFA leo.
Pia mshambualiaji Yaya Sanogo hajasafiri kwenda uturuki kwa ajili ya mpambano huo.
Wenger amesema anatamani kupambana na timu zilizo juu zaidi barani ulaya.
Leo Arsenal itacheza mechi ya kwanza dhidi ya Basiktas nchini Uturuki.
Arsenal iliitoai klabu nyingine ya Uturuki Fenerbahce katika hatua ya makundi msimu uliopita.
0 comments:
Post a Comment