Tuesday, 19 August 2014

Mourinho awatuhumu Barcelona asema ilishindwa kumtumia Fabregas.

Kocha mkuu wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho ameituhumu klabu ya  Barcelona kwa kushindwa kumweka  Cesc Fabregas katika nafasi nzuri uwanjani baada ya kiwango chake kuimarika zaidi ndani ya Chelsea.
Mhispania huyo alijiunga na Chelsea kwa uhamisho wa  € million 45 mapema msimu huu, na jana alisaidia timu yake kupata ushindi wa mabao  3-1 dhidi ya  Burnley.
Barcelona  iliamua kumuuza Fabregas ikidai kuwa kiwango chake kiliporomoka lakini  Mourinho amedai kuwa Baka hawajui jinsi ya kumtumia Cesc.
Mourinho amesema kuwa kama mchezaji ni chaguo la kwanza ni vigumu kufanya makosa,amesema kuwa Fabregas ni chaguo lake halali na anamjua vizuri baada ya kuwanaye katika ligi ya Hispania.
Burnley ilitangulia kufunga lakini Chelsea ilizinduka na kocha huyo akadai kuwa  Fabregas na Nemanja Matic walifanya kazi kubwa mno.
Wachezaji waliofunga mabao jana ni mshambuliaji mpya Diego Costa aliyefunga dakika ya 17, Andre Schrulle dakika ya 21 na Branislav Ivanovic dakika ya 34.
Scott Arfield alitangulia kuwafungia wenyeji mapema dakika ya 14 kabla ya The Blues kugeuza kibao na kuibuka na ushindi huo mnene ugenini, wachezaji wapya wengine Thibaut Courtois na Didier Drogba wakicheza pia.

0 comments:

Post a Comment