Kikosi cha Tanzania All Stars chatangazwa,kucheza na Real Madrid.
Magwiji wa klabu ya Real Madrid ya Hispania watakuja Tanzania Agosti 22 ili kucheza na kikosi maalum cha wachezaji nyota wa Tanzania(Tanzania All Stars) mchezo utakaopigwa Agosti 23 mwaka huu.Katika ziara hiyo pia watafanya utalii katika vivutio mbalimbali, ikiwemo kupanda mlima Kilimanjaro.
Real Madrid inakuja nchini kwa mwaliko wa kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN), chini ya Mkurugenzi wake Mkuu, Farough Baghozah.
Kuelekea mchezo huo kikosi cha Tanzania All Stars Kimetajwa na itakuwa Chini ya makocha Charles Boniface Mkwasa ‘Master’ na Wasaidizi Freddy Felix Minziro na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, Daktari Mwanandi Mkwankemwa
Viongozi ni Mtemi Ramadhani, Hassan Mnyenye, Omar Gumbo na Hamisi Kisiwa.
Kikosi hicho kitaingia kambini Dar es Salaam kujiandaa kwa mchezo huo Utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji ni makipa Mwameja Mohamed na Manyika Peter,mabeki Nsajigwa Shadrack, Mecky Mexime, Boniface Pawasa, John Mwansasu,
Abubakar Kombo, George Masatu, Habib Kondo,
Viungo Suleiman Matola, Shaaban Ramadhani, Salvatory Edward, Sabri Ramadhani ‘China’, Yussuf Macho, Abdul Mashine, Abdul Maneno, Mao Mkami, Steven Nyenge, Madaraka Suleiman, Akida Makunda na Mtwa Kihwelo.
Washambuliaji ni Monja Liseki, Iddi Moshi, Dua Said, Emmanuel Gabriel, Said Maulid, Thomas Kipese, Nasor Mwinyi ‘Bwanga’, Edibilly Lunyamila, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’, Clement Kahbuka,
Madaraka Suleiman na Akida Makunda.
Miongoni mwa nyota wanaotarajiwa kuja na Real nchini ni pamoja na Wanasoka Bora wa zamani wa Dunia, Mfaransa Zinadine Zidane, Mreno Luis Figo na Mbrazil, Ronaldo Lima.
Magwiji hao wa Real tayari wamekwishafanya matangazo ya ziara yao nchini wakisema wana hamu mno ya kukanyaga ardhi ya Tanzania.

0 comments:
Post a Comment