Wednesday, 20 August 2014

Kozi ya ukocha leseni A itafanyika Septemba 4

Kozi ya ukocha wa Leseni A inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) itafanyika mara ya kwanza nchini, jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 4 mwaka huu.
Mkufunzi wa kozi hiyo itakayofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume atatoka CAF, na itamalizika Septemba 8 mwaka huu wakati ada ya ushiriki ni sh. 300,000.
Washiriki wa kozi hiyo ni wale wenye leseni B ya ukocha ya CAF.
Fomu kwa ajili ya ushiriki wa kozi hiyo zinapatikana kwenye ofisi za TFF na tovuti ya TFF

0 comments:

Post a Comment