Mambo yameiva maombi AFCON 2017,Kenya wapeleka maombi,wasema wataandaa na Tanzania.
Kenya na Ethiopia wametangaza nia ya kuandaa michuano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika za Mwaka 2017, AFCON 2017, Baada ya Shirikisho la Soka Africa kuwanyang’anya Libya Uenyeji.
Taarifa kutoka nchini Kenya zimedai kuwa Shirikisho la soka nchini humo imewaeleza CAF kuwa wataungana na Tanzania au Uganda au Rwanda kuandaa michuano hiyo.
Ikumbukwe kuwa jana Tanzania ilitangaza nia ya kuanaa michuano hiyo huku ikidai kuwa itapeleka taarifa kule Cairo,Misri.
Akizungumza na wanahabari jana jijini Dar es salaama,katibu mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa alisema hatua hiyo inakuja baada ya kamati ya utendaji ya TFF kukutana mapema wikiendi iliyoipita.
TFF imetangaza nia ya kuwasilisha Maombi yake ya kuwa Mwenyeji wa AFCON 2017 na wamesema wataandaa Maombi hayo na kuyapeleka Serikalini ili kupata baraka za Viongozi wa Nchi kabla kupelekwa huko Cairo Makao Makuu ya CAF.
Ethiopia,walioanda michuano hiyo miaka ya 1962, 1968 na 1976,imesema itapeleka mara moja ombi hilo.
Rais wa shirikisho la soka la Ethiopia (EFF) Junedin Basha amesma kuwa wana viwanja vizuri pale Addis Ababa na Bahir Dar na wanaendelea kutengeneza viwanja vingine.
0 comments:
Post a Comment