Thursday, 28 August 2014

Malinzi Kutembelea Arusha,Kilimanjaro na Manyara.

Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manya Itapata fursa ya kutembelewa na rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi .

Katika ziara hiyo Malinzi atakutana na viongozi na kuangalia hali hali ya mpira wa miguu katika mikoa hiyo na mahitaji yake. Pia atazungumzia maono (vision) ya TFF katika mpira wa miguu.

Rais Malinzi atawasili mkoani Manyara, Agosti 29 mwaka huu, na ataanza ziara rasmi katika mkoa huo Agosti 30 mwaka huu. Agosti 31 mwaka huu atakuwa Arusha, na kumalizia Septemba 1 mkoani Kilimanjaro
Katika ziara hiyo, Rais Malinzi atafuatana na Mkurugenzi Msaidizi (Wanachama) wa TFF, Eliud Mvella. Pia Septemba 8 mwaka huu, Rais Malinzi ataanza ziara ya mikoa ya Iringa, Mbeya na Njombe.

0 comments:

Post a Comment