Manchester United yatoa namba za jezi za wachezaji kwa msimu mpya.
Klabu ya Manchester United jana Usiku ilitangaza Namba za Jezi watakazovaa Wachezaji wao kwa ajili ya Msimu mpya wa Ligi Kuu Uingereza wa 2014/15.Mchezaji mpya Luke Shaw amepewa Jezi Namba 3 na mpya mwenzake Ander Herrera atavaa Jezi Namba 21.
Nyota Chipukizi, Adnan Januzaj, yeye amepewa Jezi Namba 11 ambayo kwa muda mrefu sana ilikuwa ikivaliwa na Ryan Giggs ambaye alistaafu mwishoni mwa Msimu uliopita na sasa ni kocha Msaidizi chini ya Mkocha mpya Louis van Gaal.
Hadi sasa Jezi Namba 7 ambayo walivaa magwiji George Best, Bryan Robson, Eric Cantona na Cristiano Ronaldo, haina Mtu.
Na nyingine ambazo hazikupewa Mtu ni Namba 5 na 9.
Katika Taarifa yao wakitangaza Namba hizi za Jezi, Klabu ya Man United imefafanua kuwa Namba ambazo hazina Mtu zitapewa Wachezaji wapya.
NAMBA ZA JEZI KWA MSIMU MPYA 2014/15:
1. De Gea
2. Rafael
3. Shaw
4. Jones
6. Evans
8. Mata
10. Rooney
11. Januzaj
12. Smalling
13. Lindegaard
14. Chicharito
16. Carrick
17. Nani
18. Young
19. Welbeck
20. van Persie
21. Herrera
22. Powell
23. Cleverley
24. Fletcher
25. Valencia
26. Kagawa
28. Anderson
29. Zaha
30. Varela
31. Fellaini
34. Lawrence
35. Lingard
36. Vermijl
38. M Keane
39. Thorpe
40. Amos
41. James
42. Blackett
45. Petrucci
46. Rothwell
48. W Keane
49. Wilson
50. Johnstone

0 comments:
Post a Comment