Manuel Almunia astaafu soka moja kwa moja,ugonjwa wa moyo umekatiza safari ya soka.
Golkipa wa zamani wa klabu ya Arsenal Manuel Almunia amestaafu kucheza soka baada ya kugundulika kuwa ana maradhi ya moyo.
Mhispania huyo mwenye miaka, 37,aliitumikia klabu ya
Arsenal miaka minane kuanzia mwaka 2004 na 2012, baadaye akajiunga na klabu ya Watford lakini mwanzoni mwa mwezi huu alijiunga na Cagliari ya Italia.
Lakini muda mfupi uliopita klabu hiyo imetangaza kuachana na mchezaji huyo baada ya vipimo kuonesha kuwa ugonjwa huo utampelekea hadi kifo chake.
Rais wa Cagliari Tommaso Giulini, akiongea na waandishi wa habari amesema kwamba vipimo vya wataalamu wa hospitali ya Padua vimethibitisha hilo na kudai kuwa Almunia ana tatizo la Hypertrophic Cardiomyopathy ugonjwa ambao unashambulia moyo.
Sports4lifetz inakukumbusha wachezaji mahiri waliofariki na maradhi hayo ni pamoja na mchezaji wa Sevilla
Antonio Puerta, mshambuliaji wa Hungari Miklos Feher, Mcameroon Marc-Vivien Foe, nahodha wa Espanyol Dani Jarque na nahodha wa klabu ya Motherwell.
0 comments:
Post a Comment