VPL kuanza Septemba 20,Simba na Yanga Octoba 12.
Shirikisho la soka nchini Tanzania(TFF) Limetoa ratiba ya ligi kuu soka Tanzania bara ambapo mabingwa watetezi,Azam FC wataanza na Polisi Morogoro Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam Septemba 20, mwaka huu.Ratiba hiyo inaonyesha kuwa Yanga SC waliomaliza nafasi ya pili wataanza na Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro siku hiyo.
Mbeya City waliomaliza nafasi ya tatu wataanza na JKT Ruvu ya Pwani, Uwanja wa Sokoine, Mbeya Septemba 20 na washindi wa nne, Simba SC wataanza na Coastal Union ya Tanga Septemba 21, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi nyingine za ufunguzi za Ligi Kuu zitakuwa kati ya Stand United watakaoikaribisha Ndanda ya Mtwara Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Mgambo JKT wataikaribisha Kagera Sugar Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa Prisons Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Wakongwe katika soka ya Tanzania, Simba SC na Yanga watakutana Oktoba 12, mwaka huu katika mzunguko wa kwanza, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment