Rojo ndani ya Manchester United kukamilisha usajili.
Klabu ya Manchester United imekubali kutoa Pauni Milioni 16 kumnunua beki wa Sporting Lisbon, Faustino Marcos Alberto Rojo.Rojo, ambaye ametua mjini Manchester na anatarajiwa kusaini Mkataba wa miaka minne akifaulu vipimo vya afya na kukubali vipengele binafsi vya mkataba wake.
Rojo atakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na United msimu huu baada ya Ander Herrera na Luke Shaw.
Louis van Gaal ametoa kipaumbele kwa usajili wa beki huyo mtumia mguu wa kushoto, Rojo, mwenye umri wa miaka 24, kufuatia kufungwa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya England Jumamois na Swansea.
Winga Luis Nani, aliyejiunga na United kutoka Sporting kwa Pauni Milioni 17 mwaka 2007, amerejeshwa kwa mkopo klabu yake hiyo ya zamani, ilia ni sehemu ya dili hilo la Rojo
0 comments:
Post a Comment