Silva kuichezea Manchester City hadi 2019.
Mchezaji wa kimataifa wa Hispania David Silva amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano wa kuendelea kuitumikia Manchester City, klabu hiyo imetangaza leo(Jumanne).Silva, aliyejiunga na City akitokea Valencia mwaka 2010, atabaki Etihad hadi mwaka 2019.
Akiwa Manchester City, mchezaji huyo mwenye miaka 28 ameshinda ubingwa wa Uingereza mara mbili, kombe la FA na kombe la ligi .
Baada ya kusaini mkataba huo Silva amesema kuwa kwa miaka minne wameweza kuitengeneza vizuri klabu ya City na kutawala soka la Uingereza.
City itaanza kutetea taji lake msimu huu kwa kuanza kuchza ugenini dhidi ya Newcastle Unitedsiku ya jumapili.
0 comments:
Post a Comment