Wayne Rooney nahodha mpya Manchester United.
Nyota wa kimataifa wa Uingereza , Wayne Mark Rooney ametuliwa kuwa Nahodha wa kikosi cha Manchester United na kocha Louis van Gaal.Mholanzi huyo amevutiwa shughuli ya mpachika mabao huyo wa England tangu aanze kazi Old Trafford na anaamini atakuwa chaguo sahihi kuwa kiongozi wa wachezaji wenzake katika timu.
Rooney amechukua mikoba ya nahodaha aliyeondoka Nemanja Vidic huku Darren Fletcher Akiteuliwa kuwa nahodha msaidizi.
"Kwangu, wakati wote muhimu chaguo la Nahodha," amesema Van Gaal katika tovuti ya klabu hiyo
Van Gaal ameongeza kuwa kama Rooney hata kuwepo uwanjani majukumu yake yatabebwa na Fletcher.
Katika mchezo wa kirafiki jana katika uwanja wa Old Trafford Manchester United ilifunga Valencia mabao 2-1.
United ilitangulia kupata bao kupitia kwa nahodha msaidizi Darren Fletcher dakika ya 49 kabla ya Rodrigo kuisawazishia Valencia dakika ya 71.
Marouane Fellaini aliyefunga bao la ushindi dakika ya 90 lakini Wayne Rooney alikosa penalti kipindi cha kwanza iliyookolewa na Diego Alves.
0 comments:
Post a Comment