Tanzania yaomba kuandaa AFCON 2017,Wambura mkurugenzi mpya mashindano TFF.
Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) Limetangaza nia ya kuandaa michuano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika za Mwaka 2017, AFCON 2017, Baada ya Shirikisho la Soka Africa kuwanyang’anya Libya Uenyeji.CAF ilifuta Uenyaji wa Libya kutokana na Vita inayoendelea Nchini humo ambayo imesababisha kutojengwa kwa Viwanja vilivyoahidiwa kwa ajili ya Fainali hizo zinazoshirikisha Nchi 16.
Kufuatia hata hiyo, Juzi CAF ilitoa nafasi kwa Nchi nyingine za Afrika kuwasilisha maombi yao ya kuwa Wenyeji na Maombi hayo yanatakiwa yawafikie CAF kabla ya Septemba 30.
Akizungumza na wanahabari jana jijini Dar es salaama,katibu mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa alisema hatua hiyo inakuja baada ya kamati ya utendaji ya TFF kuktana mapema wikiendi iliyoipita.
TFF imetangaza nia ya kuwasilisha Maombi yake ya kuwa Mwenyeji wa AFCON 2017 na wamesema wataandaa Maombi hayo na kuyapeleka Serikalini ili kupata baraka za Viongozi wa Nchi kabla kupelekwa huko Cairo Makao Makuu ya CAF.
Awali Libya walitakiwa wawe Wenyeji wa Fainali hizo Mwaka 2013 lakini kutokana na Vita hiyo wakabadilishana na Afrika Kusini waliokuwa Wenyeji wa AFCON 2013 na wao Libya kuchukua AFCON 2017.
Mashindano yajayo ya AFCON 2015 yatafanyika huko Nchini Morocco Januari 2015 na sasa Nchi zipo hatua ya Makundi kusaka Nchi 15 zitakazojumuika kwenye Fainali na Wenyeji Morocco.
Wakati huohuo TFF limetangaza rasmi kuwa kwa sasa Mkurugenzi mashindano wa shirikisho hilo atakuwa Boniface Wambura.
Wambura alikuwa msemaji wa TFF na sasa msemaji mpya anahitajika ndani ya TFF.
0 comments:
Post a Comment