Angel Di Maria kusaini leo Manchester United kwa paundi mil 59.7
Klabu ya Manchester United wamekubali kutoa pauni milioni 59.7 kumsajili Angel Di Maria kutoka Real Madrid, na kuvunja rekodi ya uhamisho ya Uingereza.Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina, 26, yuko mjini Manchester na atafanya vipimo vya afya siku ya Jumanne, kabla ya kukamilisha uhamisho ambao, ukithibitishwa utafikisha pauni milioni 132 zilizotolewa na Manchester United msimu huu kusajili wachezaji.
Huenda Di Maria akacheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Burnley siku ya Jumamosi, mchezo wa ligi kuu.
Manchester United mara ya mwisho walivunja rekodi ya Uingereza ya uhamisho mwaka 2002 walipotoa pauni milioni 29.1 kumsajili Rio Ferdinand kutoka Leeds United.
Uhamisho huu wa Di Maria umeifanya Man United itumie Jumla ya Pauni Milioni 132 kusaini Wachezaji wapya katika kipindi hiki cha Uhamisho.
Wachezaji wengine walionunuliwa na Man United katika kipindi hiki ni beki wa Kushoto Luke Shaw, Kiungo Ander Herrera na Mchezaji mwingine wa Argentina Marcos Rojo walionunuliwa kwa Jumla ya Pauni Milioni 72.
Uhamisho wa Di Maria umevunja ile Rekodi iliyowekwa na Chelsea Mwaka 2011 walipomnunua Fernando Torres kutoka Liverpool kwa Pauni Milioni 50.
0 comments:
Post a Comment