Wednesday, 13 August 2014

Madrid mabingwa wa Super Cup,Ronaldo apiga mabao yote

Klabu ya Real Madrid imetwaa ubingwa wa Super Cup baada ya kupata  ushindi wa 2-0 dhidi ya Sevilla, mchezo uliopigwa Uwanja wa Cardiff City mjini Cardiff na kutwaa.
Mabao yote yalifungwa na  Cristiano Ronaldo, huku bao la kwanza akifunga baada ya pasi ya  nyota wa Wales, Gareth Bale  Ronaldo alifunga bao la kwanza dakika ya 30.
Wakati bao la pili alifunga dakika ya 49 akipokea pasi ya Karim Benzema.
Baada ya mchezo kumalizika Ronaldo alisema kuwa Madrid itabeba ubingwa wa Hispania na pia kutetea taji lao la UEFA.
Huku kocha Carlo Ancelotti  akimsifu kiungo wake mpya Toni Kroos kwa kuonesha kiwango kizuri hiyo jana.

0 comments:

Post a Comment