Azarenka apata jeraha.
Mchezaji Victoria Azarenka raia wa Belarus atakosa sehemu iliyobaki ya msimu wa mchezo huo kutokana na jeraha la mguu ambalo limeharibu Ratiba yake.Mchezaji huyo ambaye ni mshindi mara mbili katika mashindano ya wazi ya Australian amekwisha kosa miezi mitano katika mwaka huu pekee na kuporomoka kutoka nafasi ya pili mpaka ya 25 katika viwango vya dunia vya mchezo huo.
Azarenka mwenye umri wa miaka 25, alifika robo fainali ya michezo ya wazi ya Marekani mwanzoni mwa mwezi huu na alipangwa kurejea uwanjani katika mashindano ya wazi ya Wuhan huko China.
0 comments:
Post a Comment