Polisi wanachunguza tuhuma za ubaguzi wa rangi dhidi ya Balotelli.
Polisi wa Merseyside wameanza kufanya uchunguzi juu ya
tuhuma za ubaguzi wa rangi aliofanyiwa mshambuliaji wa Liverpool, Mario
Balotelli katika mtandao wa kijamii wa Twita.
Taarifa kutoka kituo cha polisi cha Merseyside
imesomeka: "Tunaweza kuthibitisha kuwa maofisa wanachunguza maoni ya
kibaguzi yaliyotolewa kwa Balotelli katika mtandao wa Twita ".
Balotelli alishitushwa na kipigo
walichopata United, muda mfupi baada ya timu yake ya Liverpool
kutandikwa mabao 3-1 dhidi ya West Ham siku ya jumamosi na alitweet: : 'Man Utd...LOL' akijibu kipigo cha mabao 5-3 katika uwanja wa King Power Stadium.
Polisi wamesema kuna namba zimekamatwa na zitafanyiwa kazi.
0 comments:
Post a Comment