Thursday, 11 September 2014

Cameroon yainyamazisha Ivory Coast 4-1,pata matokeo mengine.

Timu ya taifa ya Cameroon imewachapa Ivory Coast mabao 4-1, Mabao hayo yamefungwa na  Clinton Mua Njie na Vincent Aboubakar, ambapo kila mtu amefunga mabao mawili.

Bao lao pekee lilifungwa kupitia Yaya Toure kwenye Mechi ya Kundi D.

Huo ni ushindi wa pili kwa Cameroon wakati Ivory Coast wameshinda moja na kufungwa moja.
Toka Kundi A, baada ya kuichapa Ugenini Nigeria mabao 3-2,  Congo wakiwa Nyumbani wameifunga Sudan mabao 2-0 ambao hicho ni kipigo chao cha pili baada kufungwa 3-0 wakiwa kwao Khartoum na Afrika Kusini Ijumaa iliyopita.


MATOKEO MENGINE
Group A
  • Congo 2-0 Sudan
  • South Africa 0-0 Nigeria
Group B
  • Malawi 3-2 Ethiopia
  • Algeria 1-0 Mali
Group C
  • Angola 0-3 Burkina Faso
  • Lesotho 1-1 Gabon
Group D
  • Cameroon 4-1 Ivory Coast
  • Sierra Leone 0-2 DR Congo
Group E
  • Togo 2-3 Ghana
  • Uganda 2-0 Guinea
Group F
  • Mozambique 1-1 Niger
  • Cape Verde 2-1 Zambia
Group G
  • Botswana 0-2 Senegal
  • Egypt 0-1 Tunisia

0 comments:

Post a Comment