Kocha wa Misri hatafukuzwa-Allam.
Mwenyekiti wa chama cha soka cha Misri, Gamal Allam amemhakikishia kocha mkuu wa timu ya Taifa ya nchi hiyo, Shawky Gharib kwamba hatafukuzwa.Mafarao walipoteza mechi ya pili ya kufuzu AFCON 2015 baada ya kufungwa na Tunisia na kupunguza matumaini ya kusonga mbele katika safari hiyo ya Morocco.
Misri walifungwa 2-0 katika mechi ya kwanza ya makundi dhidi ya Senegal.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa Shawky Gharib hataondoka katika nafasi yake na ataendelea kuwa kocha wa Mafarao.
Mashabiki wa Misri waliohudhuria mechi hiyo walikitaka chama cha soka nchini humo kumfukuza kazi kocha mkuu.
Misri itacheza mechi nyingine dhidi ya Botswana mwezi Oktoba mwaka huu.
Mafarao hawajawahi kufuzu AFCON tangu walipotwaa ubingwa mwaka 2010 nchini Angola.

0 comments:
Post a Comment