Thursday, 4 September 2014

Djockovic atinga nusu fainali,Murray akubali kushindwa.


Mcheza tennis namba moja duniani Novak Djokovic alimshinda Andy Murray katika mchezo mkali katika michuanoi ya  US Open na kufanikiwa  kuingia nusu fainali.

Djockovic alishinda kwa seti tatu kwa moja 7-6 (7-1) 6-7 (1-7) 6-2 6-4 dhidi ya Murray katika mchuano wa saa tatu na nusu na kumalizikia saa saba na dakika 17 usiku,.
Serena William
Katika nusu fainali Djokovic atachuana na Mjapani Kei Nishikori siku ya Ijumaa.
Kushindwa kwake Murray kuna maanisha kwamba hakuweza kufaulu kucheza nusu fainali ya michuano yoyote tangu afanyiwe upasuaji wa mgongo Septemba 2013.

Baada ya mchezo kumalizika Murray alisema kuwa anampongeza sana mpinzani wake kwani alikuwa bora sana.

Serena William
Katika michuano ya wanawake bingwa mara tano wa US Open Serena Williams amefanikiwa  kuingia nusu fainali ya michuano hiyo kwa kumshinda Mtaliano Flavia Pennettaseti kwa seti mbili 6-3 6-2.

Ekaterina Makarova wa Urussi naye pia aliingia  nusu fainali ikiwa mara yake ya kwanza kufika hatua hiyo katika michuano mikubwa ya kimataifa. Alimshinda Victoria Azarenka 6-4 6-2.

0 comments:

Post a Comment