Munich,Roma na Barcelona mambo poa UEFA,pata matokeo mengine.
Wakiwa wanapewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika ligi ya mabingwa Ulaya klabu ya Chelsea wakiwa katika Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London wametoka Sare ya 1-1 na Timu ya FC Schalke 04 kutoka Ujerumani.Chelsea walipata Bao lao katika Dakika ya 11 baada ya Cesc Fabregas kuunasa Mpira katikati ya Uwanja na kumpa Eden Hazard ambaye alimrudishia Fabregas aliyefunga Bao ambalo Schalke liliwakera kwani Fabregas alionekana kumchezea Faulo Max Meyer.
Dakika ya 62,mholanzi Klaas-Jan Huntelaar akaisawazishia Bao Schalke kwa Mpira ulioanza kwa kupokonywa Cesc Fabregas.
Hadi mwisho Chelsea 1 Schalke 1.
Kule Allianz Arena Jijini Munich, Wenyeji Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich walicheza Mechi yao ya kwanza ya Kundi E duhidi ya Mabingwa wa Uingereza Manchester City na matokeo ni ushindi kwa Bayern wa Bao 1-0.
Bao pekee na la ushindi kwa Bayern Munich lilifungwa na Beki Jerome Boateng katika Dakika ya 89 kwa Shuti kali toka Mita 15 kufuatia Krosi ya Nahodha Philipp Lahm.
MATOKEO MENGINE
Jumatano Septemba 17
KUNDI E
Bayern Munich 1 Man City 0
AS Roma 5 CSKA Moscow 1
KUNDI F
Ajax 1 Paris St-Germain 1
Barcelona 1 APOEL Nicosia 0
KUNDI G
Chelsea 1 FC Schalke 1
NK Maribor 1 Sporting Lisbon 1
KUNDI H
Athletic Bilbao 0 Shakhtar Donetsk 0
FC Porto 6 BATE Borisov 0
0 comments:
Post a Comment