Januzaj apiga 3 Manchester United ikishinda 4-0 dhidi ya Sunderland.
Mchezaji Adnan Januzaj alisaidia klabu ya Manchester United baada ya kuifungia mabao matatu 'hat-trick' katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Sunderland katika michuano ya vijana
chini ya miaka 21 (U 21).
Januzaj alifunga magoli hayo mbele ya Van Gaal aliyeambatana na mke wake kipenzi.
Mwishoni mwa wili iliyopita,nyota huyo kinda raia wa Ubelgiji alicheza dakika nane katika ushindi wa 4-0 dhidi ya QPR.
Januzaj atakabiliwa na changamoto ya namba Old Trafford msimu huu kufuatia kutua kwa Di Maria, Ander Herrera na Radamel Falcao - lakini akicheza mbele ya Van Gaal jana, alionesha kipaji cha hali ya juu.

Adnan Januzaj akifunga goli na kuufanya
ubao usomeke 4-0

Anderson akimpongeza Adnan Januzaj baada ya kufunga goli safi

Louis van Gaal na mke wake Truus
waliitazama mechi kati ya Manchester United dhidi ya Sunderland
iliyopigwa uwanja wa Old Trafford

Makocha wasaidizi wa Man United, Stuivenberg na Ryan Giggs wakishuhudia.
0 comments:
Post a Comment