Juventus yaitandika AC Milan
Ligi kuu ya Italia iliendelea kurindima jana na mchezo uliokuwa unasubiriwa kwa hamu ni mchezo baina ya AC Milan na Juventus,uwanja wa San Siro.Mabingwa hao wameibuka na ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Milan bao la Dakika ya 71 la Carlos Tevez .
Ushindi huo umeifanya Juventus sasa ishike uongozi wa Ligi hiyo ya Italia wakiwa na Pointi 9 kwa Mechi 3.
Pia, ushindi huo ni kisasi cha kocha wa Juve, Massimiliano Allegri, ambaye Mwezi Januari alifukuzwa kazi na AC Milan.
Serie A inaendelea Leo kwa Timu nyingine zote kuingia dimbani.
Jumapili Septemba 21
Atalanta v Fiorentina
Chievo v Parma
Genoa v Lazio
AS Roma v Cagliari
Sassuolo v Sampdoria
Udinese v Napoli
Torino v Verona
Palermo v Inter
0 comments:
Post a Comment