Madrid yapiga 8-2 Ronaldo atupia hat-trick
Mchezaji bora wa dunia Cristiano Aveiro Ronaldo amepiga hat-trick wakati klabu ya Real Madrid ikibamiza Deportivo la Coruna mabao 8-2 katika La LIga Uwanja wa Riazor.Ronaldo alifunga mabao yake katika dakika za 29, 41 na 78, wakati mabao mengineya Real yamefungwa na James Rodriguez dakika ya 36, Gareth Bale dakika ya 66 na 74 na Javier Hernandez ‘Chichairto’ dakika ya 88 na 90.
Deportivo ilipata mabao yake ya kufutia machozi kupitia kwa Haris Medunjanin na Jose Verdu Nicolas.
Hilo inakuwa hat trick ya 23 kwa Ronaldo.

0 comments:
Post a Comment