Sunday, 28 September 2014

Loic Remy-Liverpool wamenitangaza vibaya,'mimi siumwi'.

Mshambuliaji wa  Chelsea Loic Remy amethibitisha Liverpool ilikataa kumsaini kwa sababu ya matatizo ya afya wakitaja Moyo na hilo limemchukiza kwa kutangazwa vibaya.

Remy, ambaye alikuwa kwenye Kikosi cha Ufaransa kilichocheza huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia Mwezi Juni na Julai, mwanzoni mwa Msimu ilikuwa aihame Klabu yake QPR kwenda Anfield lakini Dili hiyo ikafa huku Liverpool ikitangaza Mchezaji huyo ameshindwa upimwaji Afya yake.

Baadae, mwanzoni mwa Msimu, Remy akahamia Chelsea ambako kocha wake Jose Mourinho alisema ameshangazwa na uamuzi wa Liverpool wa kumtangaza Remy ana tatizo la Afya wakati Madaktari wao na wa Timu ya Taifa ya Ufaransa  walithibitisha yuko fiti kabisa.

Hivi sasa Remy ameibuka na kuonyesha masikitiko yake hasa kitendo cha Liverpool kumtangaza vibaya.

Remy amesema alikwenda Liverpool na kupimwa Afya na kila kitu kilikuwa sawa.

Remy aliongeza kuwa Baadaye Liverpool  wakataka kunipima Moyo na kisha kumwita Mtaalam ambaye akasema hakubaliani nao.
Mchezaji huyo amesema Si haki kwa Liverpool kumtangaza kuwa ana tatizo la Afya.

Aliongeza na kusema kuwa Kama walikuwa hawataki kumsainisha  ni sawa tu lakini si haki kutangazwa Magazetini na kufanya Klabu zote zimuogope.

0 comments:

Post a Comment