Thursday, 25 September 2014

VPL kuendelea jumamosi hii,Phiri asema mashabiki Simba wasiwe na hofu.

Kocha  Mkuu wa Simba, Mzambia Patrick Phiri, amewatoa hofu Wanachama na Mashabiki wa Klabu hiyo, kuwa wasikate tamaa na matokeo yaliyopita kwani sasa wamejipanga kufanya mazuri katika mchezo wake ujao dhidi ya Timu ya Polisi Morogoro, utakaofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza Jana kutokea Visiwani Zanzibar, Phiri alisema licha ya Kikosi chake kuandamwa na majeruhi wengi, lakini ana matumaini ya mchezo ujao kuwa Kikosi chake kitafanya vizuri kutokana na maandalizi yao.
Phiri alisema kuna makosa ameyafanyia kazi, ambayo ana uhakika yatakuwa yameisha na kushinda mchezo ujao.

Akizungumzia mchezo wake uliopita, alisema kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Coastal Union haikuwa lengo lake, licha ya kuwa soka lina matokeo ya aina tatu.

Kikosi cha Simba kilikwenda kuweka kambi Visiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo huo, ambapo kinatarajiwa kurejea jijini leo kwa ajili ya mchezo huo.
LIGI KUU VODACOM
RATIBA
Septemba 27
Simba v Polisi Moro [Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam]
Mtibwa Sugar v Ndanda FC [Manungu, Morogoro]
Azam FC v Ruvu Shooting [Azam Complex, Dar es Salaam]
Mbeya City v Coastal Union [Sokoine, Mbeya]
Mgambo JKT v Stand United [Mkwakwani, Tanga]

Septemba 28
JKT Ruvu v Kagera Sugar [Azam Complex, Dar es Salaam]
Yanga v Prisons [Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam]

0 comments:

Post a Comment