Sunday, 28 September 2014

Madrid na Barcelona mambo safi La Liga

Klabu Ya Real Madrid ikicheza Ugenini  katika uwanja wa  El Madriga, imeibuka na ushindi wa mabao  2-0.

Wakati mpambano huo unaendelea katika Dakika ya 20 ya Mchezo huo Anga za uwanja wa  El Madriga zilivamiwa na Ndege iliyokodiwa na Kundi la Mashabiki wa Manchester United, liitwalo United Reel, huku likiwa na Bango kubwa ‘COME HOME RONALDO – UNITED REEL’.

Real walipata Bao la Kwanza Dakika ya 32 kupitia kwa Luka Modric akiwa Mita 20 na akaachia Shuti lililompita Kipa Asenjo.

Cristiano Ronaldo akapiga Bao la Pili dakika ya 40 alipounganisha Krosi ya Karim Benzema na hilo ni Bao lake la 10 kwenye La Liga Msimu huu.
Hadi mwisho Villareal 0 Real 2.

Matokeo mengine FC Barcelona waliitandika  Granada mabao 6-0 na kutwaa uongozi wa La Liga huku Neymar akipiga Hat-triki na Lionel Messi kufunga mabao 2.

Mabao ya Barcelona yalifungwa na Neymar, Dakika za 26, 45 na 66, Ivan Rakitic, 43 na Messi 62 na 82.

0 comments:

Post a Comment