Sunday, 28 September 2014

Ndege za mashabiki wa Manchester United zavamia uwanja nchini Hispania wakati Ronaldo anacheza.

Mashabiki wa klabu ya Manchester United wameendelea kumshinikiza mchezaji bora wa dunia Christiano Ronaldo ili arudi jijini Manchester ili kuitumikia klabu hiyo inayotumia uwanja wa Old Traford.

Wakati mpambano wa ligi kuu Hispania ukiendelea kati ya Villarel na Madrid   katika Dakika ya 20 ya Mchezo huo Anga za uwanja wa  El Madriga zilivamiwa na Ndege iliyokodiwa na Kundi la Mashabiki wa Manchester United, liitwalo United Reel.
Mchezo unaendelea huku ndege zikirindima,angalia juu usawa wa uwanja.


Kundi hilo la mashabiki lilitanda anga za uwanja huo  huku likiwa na Bango kubwa ‘COME HOME RONALDO – UNITED REEL’.

Kwa zaidi ya wiki mbili sasa uvumi unaendelea kuwa nyota huyo wa kireno anaweza kurudi Old Traford.

Tetesi zinadai kuwa Ronaldo ametengewa kiasi cha £ 140 million na Manchester United.

Katika mchezo huo Real walishinda 2-0 na Real walipata Bao la Kwanza Dakika ya 32 kupitia kwa Luka Modric akiwa Mita 20 na akaachia Shuti lililompita Kipa Asenjo.

Cristiano Ronaldo akapiga Bao la Pili dakika ya 40 alipounganisha Krosi ya Karim Benzema na hilo ni Bao lake la 10 kwenye La Liga Msimu huu.
Hadi mwisho Villareal 0 Real 2.
Maandishi hayo yakisomeka kwenye ndege

0 comments:

Post a Comment