Manchester United hawana hela za kuwanununua wachezaji wangu asema Guardiola.
Kocha wa klabu ya Bayern Munich, Pep Guardiola amewaonya Manchester United kuwa hawawezi kumudu kuwanunua wachezaji wake bora na amedai hataki kuona nyota wake kama Arjen Robben, Bastian Schweinsteiger na Thomas Muller wanakwenda kucheza ligi kuu Uingereza.Pep aliulizwa jana mchana kama aliwahi kumkataliwa Louis van Gaal kusajili wachezaji wake, Guardiola alitikisa kichwa na kusema: klabu ya Manchester United haikuwa na hela za kutosha.
Van Gaal akipochukua hatamu Uited aliahidi kuwanunua wachezaji wengi hasa kutoka Munich lakini hakufanikiwa kumnasa hata moja kutoka Munich.
0 comments:
Post a Comment