Wednesday, 10 September 2014

Manchester United kuanika rekodi ya mapato leo.

Klabu ya Manchester United wanatarajia kutangaza rekodi ya mapato leo (Septemba 10) ambayo inakadriwa kufikia paundi milioni 420 kwa msimu uliopita, huku wakipata faida ya paundi milioni 25 kutokana na mauzo ya mamilioni ya jezi duniani kote.

Mapato hayo ya mwaka pia yatahusisha fidia waliyomlipa kocha David Moyes na benchi lake la ufundi, lakini fedha hizo hazitahusisha hasara yoyote waliyoipata baada ya kushindwa kufuzu michuano ya UEFA kwa msimu huu

Taarifa zinafafanua kuwa mapato ya jumla yanakadriwa kuwa paundi milioni 429 hadi 432, na ni ongezeko la asilimia 18 hadi 19.

0 comments:

Post a Comment