Wednesday, 10 September 2014

Ramsey hati hati kuwavaa Manchester City

Mchezaji Aaron Ramsey yuko hatarini kukosa mechi ya Arsenal dhidi ya Manchester City siku ya jumamosi baada ya kupata majeruhi ya kifundo cha mguu katika ushindi wa Wales wa mabao 2-1 dhidi ya Andorra jana usiku.

Kiungo huyo alipata majeruhi hayo baada ya kufanyiwa rafu na mchezaji wa Andorra ambapo alipatiwa matibabu, lakini akatolewa uwanjani.

Kocha wa timu, Chris Coleman alisema ukubwa wa  majeruhi utatangazwa saa 24 kuanzia jana usiku, na hali hiyo imempa maumivu ya kichwa, kocha Arsene Wenger.
In pain: Aaron Ramsey limped off injured for Wales in their 2-1 Euro 2016 qualifier win at Andorra
  Aaron Ramsey alipata majeruhi ya kifundo cha mguu

 
Going down: Ramsey picked up a suspected ankle injury while battling for the ball
  Ramsey alipata majeruhi ya kifundo cha mguu akichuana na mchezaji wa Andorra.
Hobble: Ramsey is helped to his feet by a physio but he was unable to continue in Andorra
Daktari wa Wales akimsaidia Ramsey, lakini alishindwa kuendelea na mechi
Twisted it: Chris Coleman says he hopes Ramsey's injury wasn't enough to keep him out for too long
Chris Coleman alisema anaamini majeruhi ya Ramsey haiwezi kumuweka nje ya uwanja wa muda mrefu 

0 comments:

Post a Comment