Thursday, 18 September 2014

Mandzukic atafanyiwa upasuaji wa pua.

Mshambuliaji wa Atletico Madrid Mario Mandzukic atafanyiwa upasuaji kwenye pua lake ambalo lilijeruhiwa wakati wa kichapo cha mabingwa hao wa La Liga cha 3-2 Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mikononi mwa Olympiakos ya Ugiriki Jumanne.

Raia huyo wa Croatia mwenye umri wa miaka 28 aliachwa akivuja damu kwenye pua lake baada ya kugongana na Patjim Kasami dakika ya tatu lakini alimaliza dakika zote 90 na kufunga bao lake la tatu katika mechi sita tangu ajiunge nao kutoka Bayern Munich Julai.

Mandzukic  atakosa mechi ya La Liga dhidi ya Celta Vigo Jumamosi na huenda akakaa nje wiki mbili, na hivyo kutilia shaka uwezekano wake wa kucheza mechi muhimu ya Atletico Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya nyumbani dhidi ya Juventus ya Italia Oktoba 1.

0 comments:

Post a Comment