Thursday, 18 September 2014

Majanga....Tanzania yaporomoka tena viwango FIFA,Ujerumani bado ngangari ila Uholanzi.....

Majanga Tanzania..............Tanzania imeendelea kuporomoka katika viwango vya shirikisho la soka duniani (FIFA) ikilinganishwa na ubora wa mwezi uliopita.

Taarifa zilizonaswa muda huu na Sports4lifetz ni kwamba Tanzania imeporomoka nafasi 5 kutoka nafasi ya 110 hadi nafasi ya 115.

Katika mwezi Julai Tanzania ilijitahidi kushika nafasi ya 106 na mwezi Agosti ilikuwa ya 110 lakini kwa sasa imeporomoka zaidi huku mchezo wa mwisho wakibamizwa mabao 2-0 na Burundi.

Kwa upande wa Afrika ya mashariki nchi ya Uganda inashika nafasi ya kwanza huku duniani ikiwa ya 79.

Rwanda ni ya pili ila ikishika nafasi ya 93 duniani huku Kenya ikishika nafasi ya 3 na ya 111 duniani.

Tanzania inashika nafasi ya 4 Afrika mashariki,ya 33 Afrika na ya 115 duniani.

Kwa upande wa Afrika Algeria imeendelea kuwa tishio kwa kushika nafasi ya kwanza huku duniani ikiwa ya 20.

Kwa ujumla Uholanzi imeporomoka kutoka ya 3 hadi ya 4 huku Ujerumani ikiwa ya kwanza na Argentina ikiwa ya pili na ya tatu ni Colombia.

20 BORA DUNIANI.
1 Ujerumani



2 Argentina



3 Colombia



4Uholanzi

5 Ubelgiji



6 Brazil



7 Uruguay



8 Hispania



9 Ufaransa



10 Switzerland


11 Ureno


12 Chile


13 Italy


14 Ugiriki


15 Costa Rica


16 Mexico


17 USA


18Uingereza


19 Croatia


20 Algeria.





0 comments:

Post a Comment