VPL kuanza jumamosi Azam na Polisi Moro,Yanga na Mtibwa.
Ligi kuu kandanda Tanzania Bara itaanza kunguruma jumamosi hii Septemba 20 katika viwanja mbalimbali. Mabingwa watetezi, Azam FC wakifungua dimba na Polisi Morogoro Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Yanga SC wataanza na Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro siku hiyo, wakati washindi wa tatu, Mbeya City wataanza na JKT Ruvu ya Pwani, Uwanja wa Sokoine. Mechi nyingine za ufunguzi za Ligi Kuu zitakuwa kati ya Stand United watakaoikaribisha Ndanda ya Mtwara Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Mgambo JKT wataikaribisha Kagera Sugar Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa Prisons Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani. Mabingwa wa zamani wa ligi hiyo, Simba SC wataanza kampeni ya kutwaa tena taji hilo Septemba 21 dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Raundi ya pili itaendelea Septemba 27 na 28 SIMBA SC Vs POLISI MOROGORO NATIONAL STADIUM MTIBWA SUGAR Vs NDANDA FC MANUNGU AZAM FC Vs RUVU SHOOTINGS AZAM COMPL MBEYA CITY Vs COASTAL UNION SOKOINE MBEYA MGAMBO JKT Vs STAND UNITED MKWAKWANI TANGA 28.09.2014 JKT RUVU Vs KAGERA SUGAR AZAM COMPLEX DAR ES SALAAM YOUNG AFRICANS Vs TANZANIA PRISONS NATIONAL STADIUM | |||||||||||||||||
0 comments:
Post a Comment