Mashindano ya Big Brother yasogezwa mbele,moto wateketeza nyumba.
Uzinduzi wa makala mapya ya kipindi maarufu cha Big
Brother nchini Afrika Kusini umeahirishwa baada ya moto mkubwa
kuteketeza studio za kipindi hicho mjini Johannesburg.
Washiriki katika kipindi hicho kutoka nchi 14 Afrika watakuwa wanashiriki katika makala ya 9 ya kipindi hicho.
Kipindi chenyewe kinatarajiwa kupeperushwa kwa siku 99 kabla ya mshindi kutangazwa.

0 comments:
Post a Comment