Kufuzu AFCON 2015 Ghana chupuchupu mbele ya Uganda,Pata Matokeo yote.
Mechi za Makundi kuwania kuingia Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika huko Morocco Mwakani, AFCON 2015, zimeendelea jana ambapo Mabingwa Watetezi Nigeria wakiwa kwao Mjini Calabar walihenyeshwa 3-2 na Congo Brazzaville.Nigeria ndio walitangulia kupata Bao Dakika ya 13 Mfungaji akiwa Efe Eric Ambrose na Congo kujibu kwa mabao ya Prince Oniangue, Dakika ya 16, na mbili za Thievy Bifouma Koulossa kwenye Dakika za 41 na 54, moja likiwa Penati.
Bao la Pili la Nigeria lilifungwa na Gbolahan Salami katika Dakika ya 88 baada ya patashika.
Wakati Congo Brazzaville, chini ya Kocha Mkongwe Claude Le Roy, wakisheherekea ushindi wa Ugenini Jirani zao Congo DR, kwenye Mechi ya Kundi D, walipata machungu kwa kunyukwa Nyumbani kwao Stade Mazembe Mjini Lubumbashi mabao 2-0 na Cameroon iliyoanza himaya mpya bila Nahodha wao Samuel Eto'o, mwenye Miaka 33, ambaye amestaafu.
Clinton N'Jie, ndiye aliwapa Bao la kwanza katika Dakika za Majeruhi za Kipindi cha Kwanza..
Zikiwa zimebaki Dakika 9 Mpira kwisha, Mchezaji anaecheza Soka lake huko France, Vincent Aboubakar, aliwapa Cameroon Bao la Pili.
MATOKEO.
- DR Congo 0-2 Cameroon
- Ethiopia 1-2 Algeria
- Zambia 0-0 Msumbiji
- Nigeria 2-3 Congo Brazzaville
- Gabon 1-0 Angola
- Burkina Faso 2-0 Lesotho
- Ghana 1-1 Uganda
- Niger 1-3 Cape Verde
- Ivory Coast 2-1 Sierra Leone
- Mali vs Malawi (mchezo umeahirishwa)
- Tunisia 2-1 Botswana
Tonny Mawejje alimzidi akili Kipa Dauda na kuipa Uganda Bao katika Dakika ya 44 na Ghana kusawazisha kwa Penati ya Ayew katika Dakika ya 49.
Mechi za Makundi za AFCON 2015 zitaendelea Jumatano Septemba 10.
0 comments:
Post a Comment