Baada ya Rwanda kuondolewa kufuzu AFCON Tady/Birori afungiwa miaka miwili.
Kamati ya Maandalizi ya michuano ya kufuzu AFCON 2015 imemfungia mchezaji Etekiama Agiti Tady kwa miaka miwili baada ya kuichezea Rwanda kimakosa.Mchezaji huyo alikutwa hatua ya kutumia majina mawili tofauti na kuwa na hati mbili za kusafiri za Rwanda na Kongo na licha ya Amavubi kufuzu hatua ya makundi ya mtoano, imeondolewa kwa kosa hilo.
Katika kikao chake mjini Addis Ababa, Ethiopia Kamati hiyo imeamua kumsimamisha Etekiama Agiti Tady kwa miaka miwili.
Mchezaji huyo amekuwa akiichezea AS Vita ya kwao Kinshasa kwa pasipoti ya Kongo, wakati huo huo anaichezea timu ya taifa ya Rwanda kwa jina lingine, Dady Simeon Birori akiwa na tarehe tofauti ya kuzaliwa pia.
Rwanda iliondolewa katika hatua ya makundi kufuzu kwa kosa la mchezahi huyo.

0 comments:
Post a Comment