Ole Gunnar Solskjaer ajiuzulu kuifundisha Cardiff City.
Klabu hiyo inashika nafasi ya 17 katika timu zinazogombea kupanda EPL na juzi ilipigwa 1-0 na Middlesbrough na kupigwa mabao 4-2 dhidi ya Norwich.
Mlinzi mkongwe Danny Gabbidon na Scott Young wataiongoza klabu kwa muda.
Solskjaer alibeba mikoba ya Malky Mackay Januari 2014 wakati Cardiff ikiwa katika ligi kuu.
Mmiliki wa klabu Vincent Tan amesema kuwa walimchukua Ole Gunnar Solskjaer ili aiokoe timu isishuke daraja lakini kwa bahati mbaya Ole Gunnar Solskjaer alishindwa kuiokoa klabu hiyo.
Rekodi za Ole Gunnar Solskjaer ndani ya Cardiff . |
|---|
|
Amecheza mechi: 30 |
|
Ameshindas: 9 |
|
Sare: 5 |
| Kufungwa: 16 |

0 comments:
Post a Comment