Sunday, 14 September 2014

Real Madrid wachakazwa na Athletico Madrid.

Klabu ya Real Madrid imeendelea kuonewa na Athletico  Madrid  baada ya kutandikwa mabao 2-1 usiku wa kuamkia leo  Uwanja wa Bernabeu mjini Madrid, Hispania katika mchezo wa La Liga.

Mchezo huo ambao ulishuhudiwa kwa Kocha Diego Simeone kutazama  mchezo huo kutokea jukwaani kutokana na kuwa anatumia adhabu.

Ikumbukwe kuwa kocha huyo alifungiwa mechi 8 huku  mechi nne kwa kosa  la kuvuka mstari akiwa karibu na mwamuzi msaidizi  na mara mbili alionekana akimgonga Refa huyo nyuma ya Kichwa, michezo miwili baada ya kugoma kutoka, mchezo moja baada ya kupiga makofi wakati akipewa adhabu hiyo na mchezo moja kwa kosa la kubaki uwanjani kwa muda badala ya kutoka uwanjani baada ya vurumai hiyo.

Atletico Madrid ilipata bao la kuongoza dakika ya 10 tu kupitia kwa Tiago kabla ya Real Madrid kusawazisha dakika 16 baadaye kupitia kwa Cristiano Ronaldo aliyefunga kwa penalti. 
Arda Turan aliifungia bao la ushindi Atletico dakika ya 76 akimalizia kazi nzuri ya Raul Garcia.

Hii ni mara ya kwanza  kwa Atletico kuwafunga mfululizo majirani zao hao wa Madrid.

0 comments:

Post a Comment