Sunday, 14 September 2014

Azam Kutumia 4-4-1-1 Yanga 4-4-2,mchezo ngao ya jamii leo

Azam na Yanga watapambana leo kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii   Uwanja wa Taifa  kuashiria ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania.

Mchezo huo utaanza  majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Yanga ikiwa  na rekodi ya kufanya vizuri katika michezo ya Ngao ya Jamii, itashuka dimbani kupambana na wana lambalamba Azam FC huku ikiwa na kumbumbuku ya ushindi katika mchezo wa Ngao ya Jamii msimu uliopita ambapo watoto wa Jangwani waliibuka na ushindi wa bao 1-0,bao la Salum Telela.

Kocha Marcio Maximo ambaye atakua akiongoza Yanga mara ya pili katika dimba la Uwanja wa Taifa  amesema vijana wake wote wapo katika hali nzuri jambo ambalo linampa wigo mpana wa kikosi kuchagua nani amtumie katika mchezo huo.
Kocha msaidizi wa Azam Ramadhani Kally Ongala amesema kuwa wako tayari kwa mchezo huo na hawataibeza Yanga.
Kuelekea mchezo huo kocha mkuu wa Azam Omog amesema atatumia mfumo wa 4-4-1-1 wakati mbrazil Maximo akitumia 4-4-2.

Mfumo huo wa 4-2-2 unaonekana kuwa na faida kubwa kwa mbrazil huyo huku Ongala akisema kuwa mwalimu Omog ni mzoefu wa kutumia 4-4-1-1.

Tayari TFF ilishatangaza viingilio vya mchezo huo kuwa ni Tshs 30,000 (VIP A) Tshs 20,000 (VIP B & C) Tshs 10,000 (Rangi ya Chungwa) na Tshs 5,000 (Bluu & Kijani).
Ununuaji wa tiketi unafanyika kwa huduma ya M-PESA au wakala CRDB  Fahari Huduma

0 comments:

Post a Comment