Ribery asema msimamo wake uko palepale,hatachezea tena Ufaransa.
Mchezaji wa klabu ya Bayern Munich,mfaransa Franck Henry Pierre Ribéry amesisitiza kuwa hana mpango wa kurudi katika soka la kimataifa baada ya kustaafu mapema kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi mbalimbali barani Ulaya.Mapema wiki hii Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya Michel Platini alisema kuwa haelewi kwanini Franck Ribery amechukua uamuzi wa kustaafu soka la kimataifa na kudai kuwa lazima aadhibiwe kama hataki kucheza.
Platini ameshangazwa sana na uamuzi huo na kudai kuwa iwapo akiitwa tena na kocha Didier Deschamps na asipojiunga na timu lazima apewe adhabu kubwa.
Ribery ambaye hakucheza fainali za kombe la dunia kule Brazil kutokana na majeraha,amesema kuwa hatarudi kucheza soka la kimataifa.
Ribery amesema kuwa aliongea na kocha Deschamps na amemweleza kuwa anataka kujikita kwenye klabu yake.
Ribery mwenye miaka 31 amecheza michezo 81 kwa Ufaransa na kufunga mabao 16.

0 comments:
Post a Comment