Thursday, 11 September 2014

Mwanamieleka O'Haire amefariki dunia.

Aliyekuwa mwanamieleka na nyota wa  WWE, Sean O'Haire amefariki dunia huko South Carolina siku ya jumanne akiwa na umri wa miaka 43.

Mwanamieleka huyo wa zamani alikutwa amefariki akiwa kwake na uchunguzi wa polisi kutoka maeneio ya Spartanburg umeeleza kuwa chanzo cha kifo bado hakijajulikana.

Kituo cha televisheni cha TMZ kimeeleza kuwa  mwili wa O'Haire umekutwa ukiwa kitandani huku ukizungushiwa kamba kwenye shingo.

Marehemu O'Haire, ambaye jina lake kamili ni  Sean Haire, alionekana mara ya mwisho siku ya jumatatu lakini jana jioni alikutwa akiwa ameaga dunia..

Kwa mara ya mwisho alicheza mchezo wa miereka mwaka  2000.

0 comments:

Post a Comment