Saturday, 6 September 2014

Ronaldinho Gaucho asaini miaka miwili nchini Mexico,kuvaa jezi namba 49.


Nyota raia wa Brazil,Ronaldo de Assis Moreira maarufu  kama Ronaldinho Gaucho amesaini mkataba wa miaka miwili wa kucheza soka katika  klabu ya  Queretaro, inayocheza ligi kuu ya Mexico Liga MX.

Mchezaji huyo mwenye miaka 34 kiungo mshambuliaji alihusishwa sana kujiunga na vilabu mbalimbali duniani baada ya kuikacha klabu ya Atletico Mineiro mwezi Julai.

Queretaro imethibitisha kumchukua mchezaji huyo wa zamani wa vilabu vya  Paris Saint-Germain, Barcelona na AC Milan,wakati  Ronaldinho ameandika kwenye ukurasa wake wa twita kuwa atavaa jezi namba 49.

Ronaldinho alibeba kombe la dunia mwaka  2002  ameshinda mataji mengi ,ni mchezaji bora wa  Fifa mara mbili na pia ameshinda mwanasoka bora wa dunia yaani  Ballon d'Or.

0 comments:

Post a Comment