Simba dimbani leo na Gormahia,Okwi ndani.
Mabingwa wa zamani wa Tanzania Simba SC watashuka dimbani leo (Septemba 6) Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kucheza Mechi ya Kirafiki na Mabingwa wa Kenya Gor Mahia.Simba ambao walibamizwa mabao 3-0 ZESCO ya Zambia katika siku ya SIMBA Itashuka uwanjani ikiwa na kocha mpya Patrick Phiri.
Sambamba na Phiri hii leo pia Okwi ataonekana kwa mara ya kwanza msimu huu akivaa jezi za Simba akitokea Yanga.
Simba pia itamtumia Mchezaji wao mpya kutoka KCB, Paul Kiongera na hii itakuwa Mechi yake ya pili kwa Simba baada ya kucheza ile waliobamizwa 3-0 na ZESCO hapo Agosti 9.
Baada ya kipigo hicho, Simba walipiga kambi huko Zanzibar na kucheza Mechi 3 za kujipima na kushinda zote.
Kesho(Septemba 7) kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Yanga watacheza Mechi ya Kirafiki na Big Bullets ya Malawi ambayo zamani ilikuwa ikiitwa Bata Bullets.
Yanga Wikiendi ijayo watafungua rasmi Msimu mpya wa 2014/15 kwa kucheza pambano la kufungua pazia kugombea Ngao ya Jamii dhidi ya Mabingwa wa Tanzania Bara Azam FC.
0 comments:
Post a Comment