RVP aliumia sana Sir Ferguson alipostafu asema Ferdinand.
Hatua ya ya Sir Alex Ferguson kustaafu kazi ya ukocha Old Trafford ilishitua kikosi kizima cha Manchester United, lakini hakuna aliyechukulia habari hizo kwa uzito wa juu kuliko Robin va Persie.Hayo ni maoni ya Rio Ferdinand ambaye amefichua siri hiyo akidai kuwa RVP alihangaika sana kuzoea hali hiyo.
Rio aliandika hayo katika kitabu cha Maisha yake kiitwacho ‘#2sides: Rio Ferdinand - My Autobiography’,
Ferguson alikuwa sababu kubwa ya Van Persie kujiunga na Man United akitokea Arsenal kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 24 mwaka 2012.
Kwa mujibu wa Rio Ferdinand, Straika wa Manchester United Robin Van Persie ndie alieumizwa sana na uamuzi wa Meneja wa zamani, Sir Alex Ferguson, kustaafu Mwaka Jana.
Ferguson alistaafu Mwezi Mei 2013 baada ya kuiongoza Man United kwa Miaka 26 na uamuzi huo ulikuja Mwaka mmoja tu baada ya Van Persie kujiunga na Man United kutoka Arsenal.
Magoli 31 ya RVP katika msimu wake wa kwanza Man United yaliwasaidia mashetani wekundu kutwaa ubingwa wa ligi kuu wakiwapora Man City.
Ferdinand aliwaambia MUTV: "Taarifa ilikuwa mbaya kwa kila mtu, lakini mtu ambaye aliumia sana kuliko yeyote ni Robin. Alijiunga mwaka mmoja kabla, alionja mafanikio na alihitaji zaidi.
"Kiukweli unaweza kuona yeye ndiye aliyeumia sana kuliko mwingine yeyote kwa muda ule".
Van Persie alihangaika katika utawala wa David Moyes msimu uliofuata na sasa yuko chini ya Mholanzi mwenzake, Lousi Van Gaal.
Kitabu cha Rio kitatoka Octoba 2 mwaka huu.

0 comments:
Post a Comment