Yanga dimbani leo kucheza na Big Bullets ya Malawi.
Klabu ya Yanga itaikabili Big Bullets FC (zamani Bata Bullets) ya Malawi leo(Septemba 7) katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam.Kuelekea mchezp huo kipa Juma Kaseja anatarajia kusimama golini Hali hiyo inatokana na mlinda mlango namba moja wa klabu hiyo, Deogratius Munish kuwa katika majukumu ya timu ya Taifa, Taifa Stars , itakayocheza mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyopo katika kalenda ya FIFA dhidi Burundu leo mjini Bujumbura.
Kocha wa makipa wa Yanga, Juma Pondamali ‘Mensah’ amesema Yanga ina makipa watatu wenye kiwango cha kuu na yeyote yule anaweza kufanya kazi nzuri uwanjani.
Katika kikosi cha pili cha Yanga mara zote langoni anasimama Kaseja, hivyo ni dalili tosha kuwa lep ndiye atakayeanza kama hatakuwa na tatizo lolote.
Tayari Big Bullets wameshatua Dar es salaam na maandalizi kwa ajili ya mechi yamekamilika.
Afisa habari wa Yanga, Baraka Kizuguto alisema wachezaji wote wapo katika morali ya juu na mechi hiyo inatarajia kuanza majira ya saa 10:00 jioni kwa mujibu wa waandaaji wa mechi DRFA.
0 comments:
Post a Comment