Wednesday, 3 September 2014

Wozniacki atinga nusu fainali US Open.

Bingwa wa zamani wa dunia Katika Tennis Caroline Wozniacki ameingia kwenye nusu fainali ya mashindano ya tennis kwa kumshinda mchezaji bora wa 13 duniani Sara Errani wa Italia kwa alama, 6-0 6-1 .

Mwanadada huy kutoka Denmark, anayeorodheshwa wa kumi miongoni mwa wachezaji bora zaidi duniani, alishinda mechi yake katika dakika 65 na kujinyakulia nafasi katika nusu fainali.

Wozniacki sasa atacheza na Peng Shuai, wa China ambaye alifika nusu fainali yake ya kwanza ya mashindano hayo kwa kumshinda
Belinda Bencic wa Usiwizi kwa seti mbili za alama 6-2 6-1.

Peng, mwenye umri wa miaka 28, alinukuliwa akisema amefurahi sana kwa kufika nusu fainali.

Katika mechi zengine za nusu fainali, ambazo zitachezwa leo, Serena Williams atamenyana na Flavia Pennetta huku Victoria Azarenka akichuana na Ekaterina Makarova.

Wozniacki, ambaye ameingia katika nusu fainali kwa mara ya kwanza katika miaka mitatu, alisema kuwa hii ni hatua kubwa sana kwake.

0 comments:

Post a Comment