Monday, 13 October 2014

Hispania,Uingereza na Sweden mambo safi kufuzu EURO 2016.

Michezo ya kufuzu EURO 2016  Iliendelea tena  Jana ambapo mabingwa watetezi Hispania walizinduka baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya  Slovakia lakini jana waliichabanga  Luxemborg mabao 4-0.

Katika mchezo huo golkipa David De Gea alidaka  badala ya Nahodha wao Iker Casillas.

Mabao ya Hispania yalifungwa na David Silva, Dakika ya 27, Paco Alcacer, Dakika ya 42, Diego Costa, 69, na Bernat, 88.

Katika Mchezo mwingine Uingereza ilipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya  Estonia kwa bao la nahodha  Wayne Rooney.

Matokeo Jumapili Oktoba 12
Austria 1 Montenegro 0 ]
Estonia 0 England 1
Russia 1 Moldova 1
Ukraine1 Macedonia 0
Luxembourg 0 Spain 4
Belarus 1 Slovakia 1
Sweden 2 Liechtenstein 0
Lithuania 0 Slovenia 2

0 comments:

Post a Comment